Jumatatu, 3 Juni 2013

 Wakwanza kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa PPFT Taifa Askofu D.Gamba wakiwa pamoja na Mwenyekiti wa PPFT Taifa
Wapili kutoka kulia ni Mwenyekiti wa PPFT Taifa Askofu Pius Erasto Ikongo. Wakwanza kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti Taifa Askofu  Wilson Mwawoga. Wakwanza kutoka kulia ni Mwenyekiti wa PPFT Mkoa wa Dar  Es Salaam, Askofu Rachel. Wapili kotoka kushoto ni Mwenyekiti wa PPFT Mkoa wa Kilmanjaro Askofu  Molar

Jumatatu, 27 Mei 2013

HUDUMA ZA ASKOFU PIUS ERASTO IKONGO AKIWA KATIKA HUDUMA MBALIMBALI


Askofu Pius Erasto Ikongo (kushoto) akimpongeza dada aliyeponywa na Bwana Yesu baada ya kuombewa na mtumishi wa Mungu katika mkutano uliofanyika Mwananyama kwa Kopa ulioandaliwa na TAG chini ya Askofu Rogate Swahi
Askofu Pius Erasto Ikongo akihubiri mkutano mkubwa katika viwanja vya Mashujaa mjini Moshi maelfu ya watu walifunguliwa na kupona
Kwaya ya TAG Kimara walipopata mwaliko wa kumwimbia Mungu katika Mkutano wa Injili uliyofanyika Milmanjaro Moshi Mjini.
Makao makuu ya Makanisa ya AG Duniani kwa hapa Tanzania ni TAG.
Askofu Pius E. Ikongo akiwa na Mtumishi mmoja wa Mungu kutoka Uganda wakiwa katika Kongamano kubwa Jiji Nairobi Kenya
Askofu Pius Ikongo akiwa na Askofu J.Kitavi  Jijini Nairobi Kenya.
Askofu P. Mwaura. Mmoja wa Wazee wa Injili hapa barani Africa akiwa na Mke wake Mama Bishop Mwaura. Wakwanza kutoka kushoto ni Askofu B.Bukuku wa Huduma ya Kweli Itakuweka HURU
Huu ni Umati mkubwa wa Watu waliofika katika Mkutano wa Neno la Mungu uliyofanyika katika Viwanja vya Mashujaa Mjini Moshi na Mungu alifanya Miujiza Mikubwa kupita kawaida baada ya Bishop Pius Ikongo Kuhubiri Neno la Mungu

ASKOFU PIUS ERASTO IKONGO AKIWA NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO TANZANIA MH. JAKAYA MRIISHO KIKWETE

MHESHIMIWA DR.JAKAYA MRISHO KIKWETE NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AKIMPA MKONO WA PONGEZI MLEZI WA UWT NA MKURUGENZI WA COMPASSION GRUP ASKOFU PIUS ERASTO IKONGO
MHESHIMIWA DR.JAKAYA MRISHO KIKWETE NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA  PAMOJA NA MAKADA MBALIMBALI WA CHAMA. WANNE KUTOKA KUSHOTO NI MKURUGENZE WA  COMPASSION GRUP, ASKOFU PIUS ERASTO IKONGO

BISHOP PIUS ERASTO IKONGO AOMBEA BUNGE LA TANZANIA


Askofu Pius Erasto Ikongo na Mwenyekiti wa Pentecoste Pastors Fellowship Taifa akiombea Bunge la Jamhuri la Muungano la Tanzania katika mkesha wa kuombea amani taifa la Tanzania ulioandaliwa na kanisa la RGC Tabata Chang'ombe katika ukumbi wa Karume PTA Tanzania siku ya tarehe 17.05.2013

Wa pili kutoka kushoto ni Askofu Pius Erasto Ikongo akiwa na watumishi wa Mungu wakati wa maombezi wa kuliombea Bunge la Taifa la Tanzania.












TANGAZO LA MKESHA WA KUOMBEA AMANI TANZANIA


Tangazo hili limetengezwa na Rumafrica



Mtume Nyaga akisoma Neno la Mungu

Wa pili kutoka kushoto ni mke wa Mtume Peter Nyaga






























 

Alhamisi, 9 Mei 2013

BISHOP PIUS E. IKONGO AWAAMBIA MAASKOFU WA PCT,CCT NA TEC SWALA LA KUCHINJA LINAHITAJI KUFIKIRI ZAIDI YA KUGAWANA MACHINJIO NA MABUCHA.



Katikati Askofu Pius Erasto Ikongo

Kotokana na Askofu Pius E Ikongo pamoja na Kanisa lake kujiondoa katika Jukwaa hilo, kumekuwa na uelewa mdogo kwa baadhi ya Maaskofu hapa Tanzania hata kupelekea kuiaminisha Jamii ya Watanzania kwamba Askofu Ikongo ni Msaliti na Anatetea Waislamu kuchinja.

Ndugu Mtanzania yako mambo mawili ambayo sikubaliani nayo katika Maaskofu hawa. La kwanza ni Kutumia Jina la Wakristo kutoa Matamko makali bila kujua Wakristo hawa maoni yao ni yapi.

Jambo la pili ni Kutoa Tamko la kugawana Machinjio na Mabucha bila kukaa na kufikiri zaidi juu ya Hasara na Faida zitakazo tokana na Tamko hilo, kwani Watanzania kwa sasa wengi ni waelewa na wasomi. Hivyo Maaskofu wakiamua kutoa matamko bila kufikiri zaidi Jamii itawaona Wamesoma ila Uzee unawapa kuamua hivyo ili kuwaachia Vijana Taifa ambalo wamekwisha libomoa.

1. TAMKO WARUMI 13 : 1--5
Nijambo lakusikitisha sana kwa Mkristo wa kweli kuanza kushabikia Viongozi hawa wa PCT ambao walianza vizuri lakini sasa wameharibika, hawafai hata kuitwa Viongozi wa PCT tena.

Misingi halisi ya Upentecoste hujishughulisha na mambo makubwa mawili, moja kutetea Neno la Mungu na kuhakikisha Maswala ya Kiroho yanachochewa ndani ya Wakristo.

Leo hii Viongozi hawa wa PCT walio vipofu wenye kuchuja mmbu na kumeza ngamia, wamefikia hatua ya Kushindana na Mkuu wa Nchi. Ebu wewe fikiria Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ameongea na Wananchi wake Tarehe 1/5/2013 Mkoani mbeya Tarehe 3/5/2013 Viongozi vipofu wanatoa Tamko la Uongo kwa maneno ya Kishetani huku wakitumia Jina la Wakristo wote Tanzania kwamba hawakubaliani na Kauli ya Mheshimiwa Rais. Jiulize tarehe 1 Mheshimiwa Rais anaongea tarehe 3 wanampinga, mbona ni muda mfupi sana? Hawa Maaskofu walikutana wapi? na lini? na walikusanya hayo maoni ya Wakristo sangapi? Najua walipigiana simu na wakakubaliana Kutoa tamko la kumpinga Mheshimiwa Rais ila wasiseme ni Wakristo wote, kwani Wakristo wa kweli wanafahamu Biblia inasema katika Warumi 13:1-4 Amwasiye mwenye mamlaka anashindana na shauri la Mungu na lazima atapata hukumu.

Ushauri wangu Viongozi wa PCT amkeni na jitoeni ndani ya Jukwaa hilo kwani Biblia katika Ufunuo 17 Jukwaa hilo linaitwa Mnyama. PCT mnatupeleka pabaya wenzenu wana AGENDA YAO YA SIRI.

2. KUGAWANA MACHINJO NA MABUCHA
Swala hili la kugawana machinjio na mabucha na rudia kusema, kama nilivyo sema mwanzo. Mimi sipingi jambo hilo bali nataka nyie Maaskofu ambao wengiwenu ni wasomi mkae na KULITAFAKARI ZAIDI ILI MTOE KAULI ILIOJITOSHELEZA. Mfano jiulizeni leo hii, tukigawana machinjio na mabucha je, Itakuaje kwenye Vyuo vikuu, Vyuo vya Majeshi, Shule za upili, Hosptal watanunua nyama zipi ? zilizo chinjwa na Waislamu au Wakristo? Nadhani kama ni kugawana machinjio na mabucha bora tungeanza na kugawana wapishi na masufuria kwanza.

Kwangu mimi naona Tatizo sio Swala la Kuchinja, bali najua na ninauhakika pamoja na ushahidi wa kutosha kwamba PCT,CCT,TEC kati yao Kuna mwenye AGENDA YAKE YA SIRI ANATAKA WENZAKE WAMSAIDIE ILI KUTIMIZA MALENGO YAKE.

Jumanne, 30 Aprili 2013

HATARI ZA JUKWAA LA KIKRISTO TANZANIA (TCF) TANZANIA CHRISTIAN FORUM KIROHO NA KITAIFA

Mtumishi wa Mungu kumekuwa na maswali mengi hasa juu ya uamuzi wangu na Kanisa letu kujitoa katika jukwaa la Kikristo Tanzania . Na wengine wamethubutu hata kusema mimi naitetea CCM au Chama Cha Mapinduzi, eti kwa vile nimesema TCF Inampango wa kuing’oa Serikali ya CCM. Kwa mawazo ya kawaida mtu lazima uwaze hivyo. Ila ukweli ni kwamba kwa mfumo wa Siasa za Tanzania Chama cha Siasa kinaondolewa na chama cha Siasa. Haiwezekani kwa Tanzania Chama Cha Siasa kikaondolewa na Dhehebu la Kidini au Kiongozi wa Kidini kwa kutumia Dhehebu lake. Nilicho maanisha ni kwamba PCT Likiwa ni moja ya baraza la Kipentecoste Viongozi wake wamekuwa Viongozi vipofu wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia. Hakuna mtu yeyote aliye Mpentecoste wa kweli mwenye Imani ya kweli atakubaliana na PCT kujiunga na TCF. Ni jambo lililo wazi kwamba Kanisa Katoliki ni tofauti kabisa na Mifumo ya CCT na PCT, PCT Viongozi wake wanaweza kujadiliana jambo la lolote la Kibiblia au la kimaendeleo na wakaamua kulitekeleza mara moja bila mjadala mwingine. Baraza la Maaskofu wa Kikatoliki hawawezi kufanya hivyo kwani wao kila kitu kimekwisha pangwa tangu Vatkan, iwe ni Mahubiri au jambo lolote la kimaendeleo au Siasa. Hivyo haiwezekani na haitawezekana hata siku moja Mpentecoste akawa kitu kimoja na Mkatoliki. Tafadhali endelea kusomo hili somo hapo chini utafahamu madhara ya TCF kimwili na Kiroho. Pia nakuomba baada ya kusoma kwa makini ujumbe huu wote kama unaswali tafadhali usisite kuniuliza niko tayari kukujibu kwa Bishop Pius Erasto Ikongo
Email: pierako@yahoo.comTel0788 171176www.bishopikongo.blogspot.com

MTEMBEO WA EKUMENI NA UJIO WA KANISA MOJA ULIMWENGUNINA TANZANIA IKIINGIA KATIKA MAANDALIZI YAKE KUPITIA (TCF)(THE ECUMENICAL MOVEMENT AND THE COMING ONE - WORLD CHURCH )‘‘Njoo, nitakuonyesha ADHABU YA YULE KAHABA MKUU, aketiye juu ya maji mengi. Na nikamwona MWANAMKE MMOJA AMEKETI JUU YA MNYAMA MWEKUNDU aliyejaa majina ya kumkufuru Mungu mwili mzima. Mnyama huyo alikuwa na vichwa saba na pembe kumi. Mkononi mwake alikuwa ameshika kikombe cha dhahabu kilichojaa mambo ya machukizo na uchafu wa uzinzi wake.


Kwenye kipaji chake cha uso palikuwa pameandikwa jina: “SIRI, BABELI MKUU,MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA DUNIA.’’.....Nikaona kuwa huyo mwanamke alikuwa AMELEWA KWA DAMU YA WATAKATIFU, yaani, DAMU YA WALE WATU WALIOUAWA KWA USHUHUDA WA YESU. ……Vile vichwa saba ni vilima saba ambavyo huyo mwanamke amevikalia. ........‘‘Yale maji uliyoyaona, yule kahaba akiwa ameketi juu yake ni jamaa za watu, makutano, mataifa na lugha. Zile pembe kumi ulizoziona, pamoja na huyo mnyama, watamchukia huyo kahaba, watamfilisi na kumwacha uchi, watamla nyama yake na kumteketeza kwa moto. Kwa maana Mungu ataweka mioyoni mwao kutimiza kusudi lake kwa kukubali kumpa yule mnyama mamlaka yao ya utawala mpaka maneno ya Mungu yatakapotimia. 18 Yule mwanamke uliyemwona ni ule mji mkubwa unaotawala juu ya wafalme wa dunia.’’(Nabii Yohana, Ufunuo 17)Unabii wa maandiko haya unaeleza juu ya mfumo wa dini ya Uasi ambapo utakuwa na nguvu katika mataifa mengi, japo ulijihusisha na mauaji ya watakatifu wengi katika Yesu Kristo.
 

Mfumo huu unaitwa Kahaba kwa vile unajihusisha na uzinzi wa kiroho, kuwa rafiki wa dunia badala ya kuwa mkweli na mwaminifu kwa Mungu. (URAFIKI KATI YA TEC,CCT,PCT) Viongozi wa PCT wanauwezo wa kuamua,kuunda,au kubuni jambo lolote kwa faida ya Wapentecoste wote Tanzania, ila TEC hawana ruhusa tena ni mwiko kwao kufanya hivyo kwani inafahamika wazi TEC inatekeleza maagizo,mipango,Mahubiri,Siasa, kama itakavyoamriwa katika Katiba na miongozo ya Vatkani na Baba Mtakatifu. Hivyo Kanisa la Pentecoste hasa Viongozi wa PCT wanatakiwa kujitoaharaka sana kwenye jukwaa hilo wanaloliita la Wakristo wote Tanzania kwa sababu Biblia inasema wazi katika 2.Wakorintho 6 : 14 — 18. PCT Ikijiondoa TCF Itakuwa imeliokoa Kanisala Pentecoste na UKAHABA WA KIROHO, la sivyo PCT itakuwa na mahusiano ya kipagani,ufisadi wa kidunia na maovu mengi; PCT ltaharibu Kanisa la kweli na kujikusanyia mali na utajiri mwingi wa dunia, huku likijiita bado kuwa ni bi-harusi wa Kristo wakati Kristo mwenyewe amelikataa (Nabii Yohana, Ufunuo 2:2:21-22).Mfumo wa ojio wa Kanisa moja Duniani inaeleweka ya kwamba Makao makuu ya Kanisa hilo kwa mujibu wa Biblia yatakuwa katika Nchi yenye vilima saba ambayo inajulikana kuwa ni Rumi. Na kwamba mfumohuu katika sehemu za mwisho utajiunga na utawala mkuu wa Kirumi utakao anzishwa na Mnyama (mpinga Kristo).Zaidi sana mfumo huu unaitwa “SIRI,BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA kwasababu ya kutumia mfumo wa kipagani na kikahaba ulioanzishwa na Nimrodi. Christmas book page 30. Na leo hii duniani kuna mifumo mikuu miwili inayoitwa ya Kikristo.Mifumo Mikubwa Ya Dini Inayoitwa Ya KikristoKatika dunia ya leo, kuna mifumo miwili mikubwa inayoitwa ya Dini Ya Kikristo. Mifumo hiyo ni Kanisa La Roman Katoliki ambalo lina jumla ya Waamini bilioni 1.3 ulimwenguni; na Baraza la Makanisa Ulimwenguni, ambalo lina jumla ya makanisa wanachama. a). Kanisa La Roman Katoliki Lilianzishwa katika karne ya 4 wakati Leo I alipotawazwa kuwa Papa wa Vatikani.Na baadaye Vatikani ikajengwa Roma na ikabakia kuwa makao makuu ya Kanisa la Roman Katoliki Ulimwenguni hadi hivi leo. Vatikani ni Nchi ndogo duniani ambayo ina ukubwa wa eneo la kilomita za mraba 0.44 (ekari 108.7 ) Mujibu wa takwimu za mwaka 1970, Vatikani inatawala Falme zaidi ya 690 milioni (sawa na heka 69) za watu Ulimwenguni. Mkuu wa Kanisa la Roman Katoliki na Utawala wa Vatikani ni Papa Francis. Kimsingi, Papa ana majina mengi; ikiwemo ya:-1) Suprime Pontif of the Universal Church2) Holy Fathers3) Primate of Italy4) ArchBishop And Metropolitani of the Romans province.5) Pontifix MaximusKiongozi huyu amekuwa akivaa kofia iliyoandikwa VICARVIS FILEII DEI ikiwa na maana ya badala ya mwana wa Mungu.b). Baraza La Makanisa Ulimwenguni (The world Council of Churches, WCC).Baraza la Makanisa Ulimwenguni lilianzishwa Amsterdam huko Uholanzi mwaka 1948 chini ya mkomunisti Dr. Eugene Carson Blake; baada ya juhudi za siku nyingi za kusaka umoja na makanisa ambayo si ya Kikatoliki. WCC inatumia neno la kigiriki “eukoumene” lenye maana ya ulimwengu unaozuia, au kataza. Mtu ambaye anakuwa katika ulimwengu huu, hawezi kuwa na uamuzi wa kueleza hisia zake, bali anatakiwa apokee mambo ya Imani na kuyakubali kuwa ni kweli kama ilivyoamuliwa na mamlaka ya Kanisa (dogma).Mkutano wa kwanza wa WCC ulihudhuriwa na wawakilishi wa madhehebu mbali mbali yenye wanachama wapatao 147 kutoka Nchi 44 Ulimwenguni. Na kabla ya mwaka 1960, wakati makao makuu ya WCC yakiwa Geneva, inaripotiwa kuwa na madhehebu wanachama 252 toka katika Nchi 83 duniani, zenye uwakilishi wa watu milioni mia nne (400,000,000).Changamoto ya kwanza ya umoja huu ilianza katika mkutano wa tatu wa WCC uliofanyika katika mji mkuu wa India New Delhi Novemba 1961, wakati WCC ilipo pokea uanachama wa makanisa ya Ki-orthodox ya Urusi , Romania , Bulgaria na Poland ambao wanaaminika kuwa walikuwa Wakomunisti.Katika mkutano wa Makanisa na Vyama uliofanyika mwaka 1969 chini ya katibu wake Mkuu Philip Alford Potter wa madhehebu ya Methodist toka visiwa vya West Indian vya Dominika, ulitoa tamko la kusema, nanukuu; “revolution should be actively promoted and supported by Christians”(Official report, p.143). Tafsiri yake kwa Kiswahili: Mapinduzi lazima yafanywe na kuungwa mkono na Wakristo. “Mapinduzi”yalikusudia kung’oa vurugu za kisiasa (za kikomunist) zilizoingizwa na wakomunisti ndani ya WCC. Hivyo Muugano wa PCT,CCT,TEC na kupata jina moja lijulikanalo kama Tanzania Christian Furum (TCF) na kwa Ushahidi wa Kimaadishi kutoka Mikoani kwa mfano TCF Mwanza, TCF Mbeya na Mazungumzo katika kikao cha tarehe 8/3/2013 yaliyoambatana na Tamko la tarehe 19 Machi 2013 kwenda kwa Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, ni wazi kwangu mimi kama Mtumishi wa Mungu Pius Erasto Ikongo na uzoefu ambao Mungu amenipa, tayari nimegundua kunamapinduzi ya Kisiasa yanayonyemelea Nchi yetu ya Tanzania kupitia Viongozi wa Kidini.Upagani aliouona Askofu Pius Ikongo Ndani Ya TCF na WCCKwa wale wanaodhani kuwa WCC au TCF ni chombo kizuri cha kuwaunganisha Wakristo bado hawaujui ukweli. WCC au TCF ni chombo cha uasi na upagani zaidi kama Ilivyojitambulisha. Baadhi ya mambo yanayodhibitisha ukweli huu ni, mkutano wa Nne wa WCC uliofanyika Upsala mwaka 1968:- 1) Mkutano huu ulimchagua Mkomunisti anayejulikana kuwa Raisi wa Baraza La Makanisa.2) WCC imejihusisha na kutoa, kugharamia, makundi ukombozi ya guelila na kigaidi yaliyo kuwepo Afrika ya Kusini na Amerika Ya kusini. Miongoni mwa makundi hayo, 19 yalikuwa Afrika na 14 ya kigaidi yalikuwa Amerika ya Kusini.3) Mwaka 1971, WCC ilimchagua mtu mwenye Imani ya Ki-Budha kuwa Katibu wa WCC huko Vietanam, Laos na Cambodia kushughulikia misaada ya Kanisa.Leo hii, kuna muongezeko wa mashirikiano kati ya WCC, Makanisa ya Roma ………. na makanisa yasiyo Roma ……. Na katika miaka ya hivi karibuni, tutashuhudia muunganiko wa makanisa yasiyo ya Ki…… kuungana na Kanisa Ka……… na kuungwa mkono na papa ili yatimie maanidko, “SIRI, BABELI MKUU,MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA DUNIA (Mtume Yohana, Ufunuo 17).Nje ya mifumo miwili mikuu inayojiita ya Kikristo na WCC, kuna mfumo mwingine ni wa Kanisa la Yesu Kristo, ………….. wale ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo (Mtume Yohana,Ufunuo 21:27). [Mfumo wa Kilokole].EKUMENITafsiri Ya EkumeniNeno Ekumeni, limetoholewa kutoka katika lugha ya kigiriki “Oikoumene”, kueleza ulimwengu unaozuia, au kataza “Inhabited World”. Mtu ambaye amekatazwa katika ulimwengu wa Ekumeni, ni Yule ambaye hawezi na hana maamuzi ya kueleza hisia zake. Awali neno hili lilitumika kumaanisha utawala wa Kirumi, lakini baadaye likaanza kutumika kumaanisha ulimwengu wote. Katika Kamusi ya Kiswahili ya TUKI, ekumeni inatajwa kuwa ni hali ya kupenda muungano wa madhehebu yote ya Kikristo; Imani au tamko la kuleta umoja wa wakristo wote. Na katika kamusi ya AMERCAN HERITAGE, Ekumeni inatajwa kuwa ni, nanukuu; A movement promoting worldwide unity among religions through greater cooperation and improved understanding. Mtembeo unaohimiza umoja wa miongoni mwa dini Ulimwenguni kwa njia ya mashirikiano na maelewano thabiti. Hata hivyo, Katika nadharia za kitheolojia, Ekumeni ni nadharia inayotumiwa na Viongozi waandamizi wa dini ya Kikristo kwa lengo la kutaka kuleta umoja wa Imani miongoni mwa makanisa au madhehebu ya Kikristo ulimwenguni. Mabaraza Ya Ekumeni UlimwenguniMabaraza ya Ekumeni ni mkutano wa maaskofu wa makanisa au madhehebu ya kidini ambao unafanyika kwa pamoja ili kujadili fundisho la Kanisa na jinsi ya kutatua athari zinazokabili utekelezaji wa mafundisho hayo katika Jamii. Awali, mabaraza ya Ekumeni yalianzishwa kwa lengo la kuamua kuweka kipimo cha Imani na sheria ambazo baada ya kukubaliwa na Baraza la Ekumeni, zitumike kuweka nidhamu katika Kanisa kwa kuzingatia maamuzi yaliyofanywa na Baraza. Kimsingi, mafunzo yaliyokuwa yanatolewa katika mabaraza ya Ekumeni ndiyo yaliainisha mkusanyiko wa kauli na hatua za adhabu kwa kila ambaye atafanya kinyume na maamuzi ya Baraza. Jambo ambalo kwa hapa Tanzania kama TCF ingekuwa imesajiliwa kisheria na kunauongozi kamili kama vile Mwenyekiti au katibu, lazima wangekaa na kutafuta ni adhabu gani waitoe kwa Askofu Pius Erasto Ikongo kwa kwenda kinyume na maamuzi ya mkutano wa tarehe 8/3/2013 katika ukumbi wa TEC kurasini Jijini Dar Es Salaam. Hata hivyo TCF haiwezi kuweka mwenyekiti au kuunda uongozi na kuwa na katiba kwasababu Katiba naUongozi uliopo Vatikan ndio TOSHA. Jambo hili kwa upande wa Makanisa ya Eastern Orthodox waliona ni mfumo wa Imani ambao umewekwa na Kanisa ili ukubaliwe na waamini kuwa ni kweli bila maswali. Na kwamba, mfumo huu unaweza kutumika katika Kanisa wakati wote, na usingefaa kutumika kwa wakati wote. Mabaraza ya Ekumeni yalianzishwa na Kanisa la Roma Katoliki kwa lengo la kutaka kukabiliana na changamoto za mgawanyiko na mtengano wa madhehebu iliyoanza kujitokeza katika Kanisa la Roma Katoliki. Tangu kutokea kwamgawanyiko kati ya Kanisa la Roma Katoliki na Kanisa la Eastern Orthodox hapo mwaka 1054 B.K., kumekuwa na mtazamo tofauti wa jinsi ya kukubaliana na mapokeo ya mafundisho yanayotokana na mabaraza ya Ekumeni. Kwanza , makanisa ya Eastern Orthodox hayajawahi kukubaliana na mabaraza yeyote yanayofanywa na Kanisa Katoliki baada ya kugawanyika; hali Kanisa la Roma Katoliki likiendelea na Mabaraza yake waliamua kuendeleza mabaraza ya Ekumeni na kuwa na Komunyo kamili chini ya Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Ulimwenguni na kuyatambua Kuwa ya Ekumeni hadi sasa. Na pili, Makanisa ya Ki-Anglikana na wale wanaoukiri U-protestanti, nayo hayakubaliani na maamuzi ya baadhi ya mabaraza miongoni mwa yale 21 yaliyokwisha kufanyika.Kwa jinsi hiyo, kumekuwa na nguvu za namna mbili kuu ambazo zinazokinzana na mabaraza ya Ekumeni; moja ni ufuasi wa Madhehebu au vikundi (sectarianism) na kutaka Kugawanya au kufanya mtenganisho (separation); nyingine ni ile inayoleta ushawishi wa ulimwengu na umoja(catholicity and unity). Hali hizi mbili, zilianza kujitokeza tangu kabla ya Kipindi cha matengenezo ya Kanisa.Hali ya Madhehebu au vikundi (sectarianism) inasababishwa na mtu wa madhehebu ambaye ana mtazamo au mawazo finyu (Mlokole wa madhehebu Fulani) katika kufuata madhehebu (au kikundi). Na akisha kufaulu anataka yeye pekee aushawishi ulimwengu wote uje nyuma yake.Kwakuwa hali ya madhehebu au vikundi na mtenganisho wa hali ya kidunia na umoja zimechangia kuondoa umoja aliosema Yesu; mtandao wa ekumeni unaleta wazo la umoja katika kupambana na kuondokana na hali hizi. Hata hivyo, mambo mengine yanayoleta mgawanyo na mtengano zaidi yamechochewa na:-1) Magomvi ya Kitheolojia: Magomvi haya yanarejea msingi wa Imani ya Kanisa la kwanza la Kristo la Mitume ( Apostolic Church ). 2) Migogoro ndani ya mtembeo wa Kanisa yanayotoka na kesi za kiitikadi na (doctrinal dispute) na sera za ki-sera (policy difference), i.e. jinsi ya kuendesha Liturjia.3) Matatizo ya Itikadi na Maadili.4) Migogoro ya Kijamii na Kiutamaduni. Mtazamo Wa Kanisa La Roma Katoliki Juu Ya Changamoto Za EkumeniKatika kukabiliana na jambo hili, Kanisa la Roma Catholic kupitia Baraza lake la Ekumeni la pili ambalo lilifanyika mjini Vatikani mwaka 1962-5 chini ya Papa Yohane wa 23; makusudi yake makuu yakiwa ni kuhuisha na kufanya matengenezo ya Kanisa Katoliki, ili kwamba mgawanyiko wa Kanisa uliotokea katika Historia usuluhishwe na kuunganishwa kwa upya, wote wawe na umoja (Yohana 17:21-23). Katika ufunguzi wa mkutano wa mtaguso wa Vatikani wa pili, Papa Yohana aliomba kusema, “Ee roho Mtakatifu fufua maajabu yako katika siku za leo, kama Pentekoste mpya” (Abott, document of Vatican II,1965). Jambo lingine la msingi ni kuwa, Liturjia ya Kanisa iliandikwa upya na mfumo wa utawala (Serikali) ya Kanisa ulibadilishwa upya katika kuufanyia matenegenzo ule uliokataliwa na wa-protestanti, ili iwe rahisi kuwaunganisha Wa-protestanti na Wakatoliki. Kimsingi, mkutano wa mtaguso wa pili uliazimia mambo matatu ambayo yatawaunganisha na makanisa mengine yasiyo ya Kikatoliki:-1) Kuwa na ibada za nyumba kwa nyumba na Bible Study kwa lengo la kuwasaidia waamini kiroho. Mikusanyiko hii ya ibada haipaswi kuwa katika ngazi ya kisomi,na itakuwa chini ya usimamizi wa Kiaskofu.2) Kudumisha mashirikiano kati ya Wakatoliki na Waprotestanti katika shughuli za Kijamii kama vile elimu, afya, maadili na matukio ya Kiutamaduni.3) Mabadilishano ya mawazo ya kitheolijia kati ya Maaskofu na Viongozi wawakilishi wa madhehebu ya dini kama msingi wa kujenga mahusiano ili kuungana upya.Mafanikio Ya Mtaguso Wa PiliSuala la kuweka mijadala na mabadilishano ya mawazo ya kitheolijia kati ya Maaskofu na Viongozi wawakilishi wa madhehebu ya dini kama msingi wa kujenga mahusiano ili kuungana upya, lilizaa matunda baada ya miaka kumi. Mwaka 1974, ilishuhudiwa kufanyika mijadala mingi Nchini Marekani kati ya Kanisa la Roma Katoliki na uwakilishi wa madhehebu, ili kupata mawazo ya kitheolojia. Miongoni mwa madhehebu yaliyoshiriki mijadala hiyo kwa mujibu wa kitabu cha “Cellebration Annivesary of the Second Vatican Council’s Degree on Ecumenism, November 21th, 1974, Wessel) ni:-1) Southern Baptist2) American Baptist3) Lutheran4) Methodist5) Epicopalins6) Presbyterians7) Reformed8) Disciple of Christ9) Eastern OrthodoxHali ya Sasa Ya Ekumeni Ulimwenguni na Tanzania Kuna mkazo mkubwa wa makanisa kutaka kuunganisha wakristo wa madhehebu yote ya Kikristo kuwa pamoja. Ujumbe unaotumika kusema haya ni kuwa, sisi hatuna tofuti............tunaweza kufanya kazi pamoja.Tuache tofauti zetu za theolojia pembeni, tunaweza kusaidiana katika kila jambo ambalo tunamua kulifanya kwa pamoja. Juhudi hizo zote zinafanywa chini ya mwamvuli wa Ekumeni, ukitasiriwa kuwa ni "waliojipanga kujaribu katika kuleta mashirikiano na umoja wa waamini wote katika Kristo" Ukiangalia kwa undani msingi wa juhudi za kuleta waamini kwa pamoja, ni ule WCC ambao ulihimizwa kwa nguvu katika miaka ya 1960; ambapo ulipoanza, Waprotestanti wa Kilibelali miongoni mwa madhehebu makubwa ya Kiprotestanti waliukataa baada ya kuona unakiuka mafundisho muhimu kama vile maandiko hayana makosa na uhalisia wa mandiko, kufufuliwa kwa mwili kwa Yesu Kristo hakutiliwi mkazo. Na kwa muda mrefu, Wa-Evangelical walijiondoa katika mfumo wa Ekumeni kwasababu ya kuhusisha makundi ambayo theolojia zao siyo sahihi, lakini roho ya kufanya mjadala imewaingia wa-evangelical na wamejikuta wamo ndani ya mfumo huu. Makanisa Wanachama Wa Baraza La Makanisa Ulimwenguni Walipo TanzaniaMabaraza Ya Kidini Tanganyika . Kwa upande wa madhehebu ya Kikristo, kuna mabaraza matatu ya madhehebu ya Kidini ambayo yanatambuliwa na Serikali toka miongoni mwa dini za Kikristo. Mabaraza yanayotambulika kisheria ni:-1. Baraza la Maaskofu wa Kikatoliki “TanzaniaEpicospical Council” (TEC). 2. Jumuiya Ya Kikristo Tanzania“Christian Council Of Tanzania ”(CCT).3. Jumuiya Ya Wapetentekoste Tanzania “Pentecostal Council of Tanzania ”(PCT). Katika siku za hivi karibuni, Viongozi wa Mabaraza ya TEC, CCT Na PCT, wameunda Jukwaa lao ambalo linaitwa Jukwaa la Wakristo Tanzania ,“Tanzania Christian Forum” (TCF).Makanisa na Mashirika ya Kiprotestanti nchini Tanzania , ambayo yamejiunga na Baraza la Makanisa Ulimwenguni (yakiwa chini ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania),hadi sasa yamefikia thelathini (30). Kabla ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania kuanzishwa mwaka 1964, wamisheni walikuwa na baraza lao la kimisheni la Tanganyika Missionary Council, ambalo lilianzishwa mwaka 1934. Makanisa Wanachama Wa Baraza La Makanisa UlimwenguniHadi sasa, kuna jumla ya makanisa matano (5), ambayo ni wanachama wa Baraza la Makanisa Ulimwenguni, “World Council Of Churches”5. Miongoni mwa makanisa haya, makanisa matatu (3) makao yake makuu yapo Tanzania ; na mengine mawili (2) hayapo Tanzania . Makanisa ambayo makao yake yapo Tanzaniani:-1. Kanisa la Anglikana Tanzania (Anglican Church of Tanzania ).2. Kanisa La Kiinjili na Kilutheri Tanzania (Evangelical Lutheran Church In Tanzania ).3. Kanisa la Moraviani (” Moravian Church in Tanzania ”)Makanisa ambayo Makao yake Hayapo Tanzania lakini yapo Tanzania ni:-1. Kanisa la Kigiriki la Kiothodox na Afrika Nzima (Greek Orthodox Patriarchate of Alexandria and All Africa)2. Dini ya Jamii ya Kirafiki (Religious Society of Friends/ Friends United Meeting).Makanisa ambayo ni wanachama wa Baraza la Makanisa Ulimwenguni yaliyopo Tanzania ni:-1. Evangelical Lutheran Church in Tanzania (ELCT)2. Anglican Church Tanzania (ACT)3. Moravian Church in Tanzania (MCT)4. Africa Inland Church Tanzania (AICT)5. Mennonite Church in Tanzania (MCT)6. Baptist Conventional Church in Tanzania7. Salvation Army8. Church of God9. Presbyterian Church of East Africa10. Kanisa la Biblia11. Mbalizi Evangelistic Church12. Methodist Church13. Christian Brethren Assembly14. African Brotherhood Church15. Tanzania Yearly MeetingNje Ya makanisa haya kumi na tano (15), kuna mashirika ya kidini yanayojihusisha na shughuli za Kanisa kwa Kiingereza “Church Related Organizations“. Kimsingi, mashirika haya siyo makanisa, lakini kwa sehemu kubwa yanafanya huduma za kikanisa kwa kushirikiana na makanisa. Mashirika ambayo ni wanachama wa Baraza la Makanisa Ulimwenguni Yaliyopo Tanzania ni:-1. Bible Society of Tanzania (BST)2. Scripture Union (SU)3. Tanganyika Christian Refugee Service (TCRS)4. Young Men’s Christian Association (YMCA)5. Young Women’s Christian Association (YWCA)6. African Evangelistic Enterprise (AEE)7. Life Ministry of Tanzania8. Mission Aviation Fellowship (MAF)9. Emmanuel International10. Habitat for Humanity11. Summer Institute of Linguistic (SIL)12. Dodoma Christian Medical Centre (DCMC)13. Mennonite Central Committee (MCC)14. United Church of Canada (UCC)15. Compassion International TanzaniaNdugu mpendwa baada ya kusoma kwa makini utakuwa umefahamu ni kwanini Askofu Pius Erasto Ikongo pamoja na Kanisa lao kuamua kujitoa TCF, na kuendelea kuwaelimisha Wapentecoste wote Tanzania kukataa kwa nguvu kubwa kujiunga na chombo hicho wanachodai ni Jukwaa la Wakristo Tanzania . Na kama wewe kweli ni Mpentecoste wa kweli utakubaliana na mimi na tuungane kwa pamoja kuwaeleza viongozi wa PCT watutoe huko kwani wanapotupeleka ni pabaya, swali ni kwanini hawa Viongozi wa PCT wasichukue maoni kwa Wachungaji wote wa Kipentecoste ndipo wachukue uamuzi wa kujiunga na TCF ? Inavyoonyesha hawa Viongozi wanataka kuchezea Roho zetu au Imani yetu. Kama hawatatangaza kuiondoa PCT ndani ya TCF, Nitakuomba uchaguzi mkuu wa Viongozi wakuu wa PCT hawa waliopo tusiwarudishe kwenye Uongozi tena. Bishop Pius Erasto Ikongo Email: pierako@yahoo.comTel 0788 171176http://www.bishopikongo.blogspot.com/ bishopikongo.blogspot.com

Jumatatu, 15 Aprili 2013

TAARIFA YA KANISA LA MIRACLE GOSPEL CHURCH IN TANZANIA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA UDINI NCHINI 13.04.2013


Siku ya Jumamosi tarehe 13.04.2013 Makamu Askofu Mkuu, Pius Erasto Ikongo aliongea na waandishi wa habari katika hoteli ya Peacock iliyoko Mnazimmoja jijini Dar es Salaam juu ya migogoro inayotekea kati ya Waislamu na Wakristo nchini Tanzania. Pia aliongelea juu ya kanisa lake la Miracle Church In Tanzania kujiengua katika JUKWAA LA WAKRISTO TANZANIA(TANZANIA CHRISTIAN FORUM (TCF)) kutokana na jukwaa hilo kushirikisha mambo ya Ukristo katika siasa na kutaka kuking'oa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Na haya ndiyo maelezo aliyoyatoa kwa waandishi wa habari.

Askofu Pius Erasto Ikongo akiongea na waandishi wa habari

TAARIFA YA KANISA LA MIRACLE GOSPEL CHURCH IN TANZANIA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA UDINI NCHINI 13.04.2013

Msomaji wa taarifa, Lelusi Kitule akisoma Press Release iliyoandaliwa na kanisa la Miracle Church In Tanzania.

Ndugu wanahabari, Tunawasalimu wote.

Tunawakaribisheni nyote katika mkutano huu muhimu kwaajili ya mustakabari wa nchi yetu. Tumewaeteni hapa kwa lengo moja tu ambalo ni kuifahamisha jamii, kupitia ninyi, namna ambavyo watu au tasisi zinazotumainiwa kuwa msaada katika kulinda na kuimairisha umoja na amani ya nchi yetu zinapogeuka kuwa chanzo cha vurugu.

Ndugu wanahabari, mnakumbuka kuwa muda wa sasa kumekuwa na mvuto baina ya dini mbili kubwa hapa nchini; Wakristo na Waislamu juu ya nani mwenye haki na kuchinja wanyama kwaajili ya kitoweo. Mnakumbuka pia mvutano huo umepanuka kiasi cha kusababisha kifo na majeruhi.

Mnafahamu pia kwamba, kabla ya mvutano wa nani mwenye haki ya kuchinja, kumekuwepo na matukio mengine ambayo yaliibuka hali ya kutiliana shaka baina ya Wakristo na Waislamu kwa upande mmoja, na Wakristo na Serikali kwa upande mwingine. Matukio hayo ni pamoja na uchomaji moto kwa makanisa, kukojolewa na kuharibiwa kwa vitabu vinavyoheshimiwa na dini hizo; yaani Biblia na Kurani.

Kutokana na hali hiyo, upande wetu Wakristo tulikubaliana kuwa madhehebu yote ya Kikristo tuungane pamoja ili tuwe na chombo cha kusaidia kudai kile ambacho tuliamini ni haki ya Wakristo. Chombo hicho kinajulikana kama JUKWAA LA WAKRISTO TANZANIA-TANZANIA CHRISTIAN FORUM (TCF)

Kwa kutambua umuhimu wa chombo hicho, sisi kanisa la Miracle Gospel Church in Tanzania, kanisa ambalo lina makanisa zaidi ya 800 chini nzima, kupitia Baraza Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (PCT) ambako ni wanachama, tuliamua kujiunga katika TCF. Tulijiunga na jukwaa hilo ili kama tulivyoamini tuweze kuutetea Ukristo na waumini walioko katika makanisa yetu.

Hata hivyo baada ya kuwa ndani ya jukwaa hilo tulishiriki vikao na mikutano mbalimbali, tumebaini mambo yafuatayo:

Mosi, Lengo la TCF kutafuta suluhisho la kero, changamoto au mambo yoyote yanayowaumiza Wakristo, bali taasisi ambayo imejigeuza kuwa chombo cha kisiasa chenye nia ya mikakati ya kuking'oa madarakani Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Pili, Tumengudua kuwa matamko ambayo yanatolewa na TCF yanahamasisha chuki na kuwafanya Wakristo kuwa watu wa visasi. Mfano ni tukio la hivi karibuni kule Tunduma mkoa wa Mbeya.

UFAFANUZI
Kutoka na ufafanuzi huo tunatoa tamko lifuatalo:
Kwamba baada ya kufanya kikao cha dharura cha tarehe 6-7/4/2013 Kamati Kuu ya Kanisa la Miracle Church In Tanzania imeamua kujitoa katika JUKWAA LA WAKRISTO TANZANIA-TANZANIA CHRISTIAN FORUM (TCF) kutokana na jukwaa hilo kutumiwa kisiasa tofauti na malengo tuliyoaambiwa. Tumefikia uamuzi huo kutokana na katiba ya kanisa letu kutuzuia kuliingiza kanisa katika harakati za kisiasa. Aidha, katika yetu inatutaka tuheshimu serikali iliyoko madarakani.

Kuhusu suala la kuchinja Kanisa la Miracle Church In Tanzania limeona hakuna madhara yoyote kwa Waislamu kuendelea kuchinja, tunawaomba waumini wa makanisayetu yote nchini pamoja na Wakristo wanaopenda amani na utulivu wa Taifa letu tuendelee kushirikiana kama ndugu kama ilivyokuwa mwanzo

Asanteni kwa kunisikiliza

Pius Erasto Ikongo
Makamu Askofu Mkuu
Miracle Gospel Church in Tanzania

MATUKIO KATIKA PICHA


Kutoka kulia ni Msomaji wa taarifa, Lelusi Kitul, katikati ni Askofu Pius Erasto Ikongo wa kanisa la Miracle Church In Tanzania, na kushoto ni Msaidizi wa Makamu wa Askofu Apostle Paul Johh

Msomaji wa taarifa, Lelusi Kitule akisoma Press Release iliyoandaliwa na kanisa la Miracle Church In Tanzania

EWE MTANZANIA MWENZANGU UNAFAHAMU YA KWAMBA TCF HAINA OFISI, HAINA MWENYEKITI,HAINA KATIBA, HAIJASAJILIWA KISHERIA, NA WAMEANZA KUTOA MATISHO MAKALI KWA SERIKALI JE, TUTAFIKA? NCHI YA KENYA INAWATAFUTA VIONGOZI WA ALSHABAB ILI WAWAKAMATE KWA KUHATARISHA AMANI NCHINI MWAO. JE, TCF WAKIHATARISHA AMANI YA NCHI YETU NYIE VIONGOZI WA SEREKALI YA TANZANIA MTAMKAMATA NANI?  NDIO SABABU SISI KANISA LETU TUMEJITOA MAPEMA, KWANI TUNADHANI TCF NI ALSHABAB YA KIKRISTO TANZANIA.

Askofu Pius Erasto Ikongo akifafanua maelezo yaliyosomwa na Msaidizi wa Askofu Lelusi Kitule
Baadhi ya waandishi wa habari waliofika katika mkutano huu. Hapa walikuwa akiuliza baadhi ya maswali kwa Askofu Pius Erasto Ikongo.
Askofu Pius Ersto Ikongo (katikati) akijiibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari Tanzania
 Kushoto ni baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini.
 Mwandishi wa Habari akiuliza Swali

Askofu Pius Ersto Ikongo akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari

Askofu Pius Ersto Ikongo akiwashukuru waandishi wa habari