Siku ya Jumamosi tarehe 13.04.2013 Makamu Askofu Mkuu, Pius Erasto
Ikongo aliongea na waandishi wa habari katika hoteli ya Peacock iliyoko
Mnazimmoja jijini Dar es Salaam juu ya migogoro inayotekea kati ya
Waislamu na Wakristo nchini Tanzania. Pia aliongelea juu ya kanisa lake
la Miracle Church In Tanzania kujiengua katika JUKWAA LA WAKRISTO
TANZANIA(TANZANIA CHRISTIAN FORUM (TCF)) kutokana na jukwaa hilo
kushirikisha mambo ya Ukristo katika siasa na kutaka kuking'oa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Na haya ndiyo
maelezo aliyoyatoa kwa waandishi wa habari.
Askofu Pius Erasto Ikongo akiongea na waandishi wa habari
TAARIFA YA KANISA LA MIRACLE GOSPEL CHURCH IN TANZANIA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA UDINI NCHINI 13.04.2013
Msomaji wa taarifa, Lelusi Kitule akisoma Press Release iliyoandaliwa na kanisa la Miracle Church In Tanzania.
Ndugu wanahabari, Tunawasalimu wote.
Tunawakaribisheni nyote katika mkutano huu muhimu kwaajili ya mustakabari wa nchi yetu. Tumewaeteni hapa kwa lengo moja tu ambalo ni kuifahamisha jamii, kupitia ninyi, namna ambavyo watu au tasisi zinazotumainiwa kuwa msaada katika kulinda na kuimairisha umoja na amani ya nchi yetu zinapogeuka kuwa chanzo cha vurugu.
Ndugu wanahabari, mnakumbuka kuwa muda wa sasa kumekuwa na mvuto baina ya dini mbili kubwa hapa nchini; Wakristo na Waislamu juu ya nani mwenye haki na kuchinja wanyama kwaajili ya kitoweo. Mnakumbuka pia mvutano huo umepanuka kiasi cha kusababisha kifo na majeruhi.
Mnafahamu pia kwamba, kabla ya mvutano wa nani mwenye haki ya kuchinja, kumekuwepo na matukio mengine ambayo yaliibuka hali ya kutiliana shaka baina ya Wakristo na Waislamu kwa upande mmoja, na Wakristo na Serikali kwa upande mwingine. Matukio hayo ni pamoja na uchomaji moto kwa makanisa, kukojolewa na kuharibiwa kwa vitabu vinavyoheshimiwa na dini hizo; yaani Biblia na Kurani.
Kutokana na hali hiyo, upande wetu Wakristo tulikubaliana kuwa madhehebu yote ya Kikristo tuungane pamoja ili tuwe na chombo cha kusaidia kudai kile ambacho tuliamini ni haki ya Wakristo. Chombo hicho kinajulikana kama JUKWAA LA WAKRISTO TANZANIA-TANZANIA CHRISTIAN FORUM (TCF)
Kwa kutambua umuhimu wa chombo hicho, sisi kanisa la Miracle Gospel Church in Tanzania, kanisa ambalo lina makanisa zaidi ya 800 chini nzima, kupitia Baraza Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (PCT) ambako ni wanachama, tuliamua kujiunga katika TCF. Tulijiunga na jukwaa hilo ili kama tulivyoamini tuweze kuutetea Ukristo na waumini walioko katika makanisa yetu.
Hata hivyo baada ya kuwa ndani ya jukwaa hilo tulishiriki vikao na mikutano mbalimbali, tumebaini mambo yafuatayo:
Mosi, Lengo la TCF kutafuta suluhisho la kero, changamoto au mambo yoyote yanayowaumiza Wakristo, bali taasisi ambayo imejigeuza kuwa chombo cha kisiasa chenye nia ya mikakati ya kuking'oa madarakani Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Pili, Tumengudua kuwa matamko ambayo yanatolewa na TCF yanahamasisha chuki na kuwafanya Wakristo kuwa watu wa visasi. Mfano ni tukio la hivi karibuni kule Tunduma mkoa wa Mbeya.
UFAFANUZI
Kutoka na ufafanuzi huo tunatoa tamko lifuatalo:
Kwamba baada ya kufanya kikao cha dharura cha tarehe 6-7/4/2013 Kamati
Kuu ya Kanisa la Miracle Church In Tanzania imeamua kujitoa katika
JUKWAA LA WAKRISTO TANZANIA-TANZANIA CHRISTIAN FORUM (TCF) kutokana na
jukwaa hilo kutumiwa kisiasa tofauti na malengo tuliyoaambiwa. Tumefikia
uamuzi huo kutokana na katiba ya kanisa letu kutuzuia kuliingiza kanisa
katika harakati za kisiasa. Aidha, katika yetu inatutaka tuheshimu
serikali iliyoko madarakani.
Kuhusu suala la kuchinja Kanisa la Miracle Church In Tanzania limeona hakuna madhara yoyote kwa Waislamu kuendelea kuchinja, tunawaomba waumini wa makanisayetu yote nchini pamoja na Wakristo wanaopenda amani na utulivu wa Taifa letu tuendelee kushirikiana kama ndugu kama ilivyokuwa mwanzo
Asanteni kwa kunisikiliza
Pius Erasto Ikongo
Makamu Askofu Mkuu
Miracle Gospel Church in Tanzania
MATUKIO KATIKA PICHA
Kuhusu suala la kuchinja Kanisa la Miracle Church In Tanzania limeona hakuna madhara yoyote kwa Waislamu kuendelea kuchinja, tunawaomba waumini wa makanisayetu yote nchini pamoja na Wakristo wanaopenda amani na utulivu wa Taifa letu tuendelee kushirikiana kama ndugu kama ilivyokuwa mwanzo
Asanteni kwa kunisikiliza
Pius Erasto Ikongo
Makamu Askofu Mkuu
Miracle Gospel Church in Tanzania
MATUKIO KATIKA PICHA
Kutoka kulia ni Msomaji wa taarifa, Lelusi Kitul, katikati ni Askofu
Pius Erasto Ikongo wa kanisa la Miracle Church In Tanzania, na kushoto
ni Msaidizi wa Makamu wa Askofu Apostle Paul Johh
Msomaji wa taarifa, Lelusi Kitule akisoma Press Release iliyoandaliwa na kanisa la Miracle Church In Tanzania
EWE MTANZANIA MWENZANGU UNAFAHAMU YA KWAMBA TCF HAINA OFISI, HAINA MWENYEKITI,HAINA KATIBA, HAIJASAJILIWA KISHERIA, NA WAMEANZA KUTOA MATISHO MAKALI KWA SERIKALI JE, TUTAFIKA? NCHI YA KENYA INAWATAFUTA VIONGOZI WA ALSHABAB ILI WAWAKAMATE KWA KUHATARISHA AMANI NCHINI MWAO. JE, TCF WAKIHATARISHA AMANI YA NCHI YETU NYIE VIONGOZI WA SEREKALI YA TANZANIA MTAMKAMATA NANI? NDIO SABABU SISI KANISA LETU TUMEJITOA MAPEMA, KWANI TUNADHANI TCF NI ALSHABAB YA KIKRISTO TANZANIA.
Askofu Pius Erasto Ikongo akifafanua maelezo yaliyosomwa na Msaidizi wa Askofu Lelusi Kitule
Msomaji wa taarifa, Lelusi Kitule akisoma Press Release iliyoandaliwa na kanisa la Miracle Church In Tanzania
EWE MTANZANIA MWENZANGU UNAFAHAMU YA KWAMBA TCF HAINA OFISI, HAINA MWENYEKITI,HAINA KATIBA, HAIJASAJILIWA KISHERIA, NA WAMEANZA KUTOA MATISHO MAKALI KWA SERIKALI JE, TUTAFIKA? NCHI YA KENYA INAWATAFUTA VIONGOZI WA ALSHABAB ILI WAWAKAMATE KWA KUHATARISHA AMANI NCHINI MWAO. JE, TCF WAKIHATARISHA AMANI YA NCHI YETU NYIE VIONGOZI WA SEREKALI YA TANZANIA MTAMKAMATA NANI? NDIO SABABU SISI KANISA LETU TUMEJITOA MAPEMA, KWANI TUNADHANI TCF NI ALSHABAB YA KIKRISTO TANZANIA.
Askofu Pius Erasto Ikongo akifafanua maelezo yaliyosomwa na Msaidizi wa Askofu Lelusi Kitule
Baadhi ya waandishi wa habari waliofika katika mkutano huu. Hapa
walikuwa akiuliza baadhi ya maswali kwa Askofu Pius Erasto Ikongo.
Askofu Pius Ersto Ikongo (katikati) akijiibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari Tanzania
Kushoto ni baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini.
Mwandishi wa Habari akiuliza Swali
Askofu Pius Ersto Ikongo akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari
Askofu Pius Ersto Ikongo akiwashukuru waandishi wa habari
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni