Katikati Askofu Pius Erasto Ikongo
Kotokana na Askofu Pius E Ikongo pamoja na Kanisa lake kujiondoa katika Jukwaa hilo, kumekuwa na uelewa mdogo kwa baadhi ya Maaskofu hapa Tanzania hata kupelekea kuiaminisha Jamii ya Watanzania kwamba Askofu Ikongo ni Msaliti na Anatetea Waislamu kuchinja.
Ndugu Mtanzania yako mambo mawili ambayo sikubaliani nayo katika Maaskofu hawa. La kwanza ni Kutumia Jina la Wakristo kutoa Matamko makali bila kujua Wakristo hawa maoni yao ni yapi.
Jambo la pili ni Kutoa Tamko la kugawana Machinjio na Mabucha bila kukaa na kufikiri zaidi juu ya Hasara na Faida zitakazo tokana na Tamko hilo, kwani Watanzania kwa sasa wengi ni waelewa na wasomi. Hivyo Maaskofu wakiamua kutoa matamko bila kufikiri zaidi Jamii itawaona Wamesoma ila Uzee unawapa kuamua hivyo ili kuwaachia Vijana Taifa ambalo wamekwisha libomoa.
1. TAMKO WARUMI 13 : 1--5
Nijambo lakusikitisha sana kwa Mkristo wa kweli kuanza kushabikia Viongozi hawa wa PCT ambao walianza vizuri lakini sasa wameharibika, hawafai hata kuitwa Viongozi wa PCT tena.
Misingi halisi ya Upentecoste hujishughulisha na mambo makubwa mawili, moja kutetea Neno la Mungu na kuhakikisha Maswala ya Kiroho yanachochewa ndani ya Wakristo.
Leo hii Viongozi hawa wa PCT walio vipofu wenye kuchuja mmbu na kumeza ngamia, wamefikia hatua ya Kushindana na Mkuu wa Nchi. Ebu wewe fikiria Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ameongea na Wananchi wake Tarehe 1/5/2013 Mkoani mbeya Tarehe 3/5/2013 Viongozi vipofu wanatoa Tamko la Uongo kwa maneno ya Kishetani huku wakitumia Jina la Wakristo wote Tanzania kwamba hawakubaliani na Kauli ya Mheshimiwa Rais. Jiulize tarehe 1 Mheshimiwa Rais anaongea tarehe 3 wanampinga, mbona ni muda mfupi sana? Hawa Maaskofu walikutana wapi? na lini? na walikusanya hayo maoni ya Wakristo sangapi? Najua walipigiana simu na wakakubaliana Kutoa tamko la kumpinga Mheshimiwa Rais ila wasiseme ni Wakristo wote, kwani Wakristo wa kweli wanafahamu Biblia inasema katika Warumi 13:1-4 Amwasiye mwenye mamlaka anashindana na shauri la Mungu na lazima atapata hukumu.
Ushauri wangu Viongozi wa PCT amkeni na jitoeni ndani ya Jukwaa hilo kwani Biblia katika Ufunuo 17 Jukwaa hilo linaitwa Mnyama. PCT mnatupeleka pabaya wenzenu wana AGENDA YAO YA SIRI.
2. KUGAWANA MACHINJO NA MABUCHA
Swala hili la kugawana machinjio na mabucha na rudia kusema, kama nilivyo sema mwanzo. Mimi sipingi jambo hilo bali nataka nyie Maaskofu ambao wengiwenu ni wasomi mkae na KULITAFAKARI ZAIDI ILI MTOE KAULI ILIOJITOSHELEZA. Mfano jiulizeni leo hii, tukigawana machinjio na mabucha je, Itakuaje kwenye Vyuo vikuu, Vyuo vya Majeshi, Shule za upili, Hosptal watanunua nyama zipi ? zilizo chinjwa na Waislamu au Wakristo? Nadhani kama ni kugawana machinjio na mabucha bora tungeanza na kugawana wapishi na masufuria kwanza.
Kwangu mimi naona Tatizo sio Swala la Kuchinja, bali najua na ninauhakika pamoja na ushahidi wa kutosha kwamba PCT,CCT,TEC kati yao Kuna mwenye AGENDA YAKE YA SIRI ANATAKA WENZAKE WAMSAIDIE ILI KUTIMIZA MALENGO YAKE.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni